“Love is not a source, it is a consequence of our understanding the divine, spiritual beginning which exists in all of us.” – Leo Tolstoy
Upendo siyo chanzo, bali ni matokeo ya kuelewa imani na uungu uliopo ndani ya kila mmoja wetu.
Ndiyo maana upendo wa kweli haubagui wala hauna vigezo.
Ni upendo ambao unaanzia ndani ya kila mmoja wetu, kwa kuelewa kile kilichopo kwa kila mmoja wetu, ambacho kinatuleta pamoja.
Upendo ndiyo nguzo kuu, iishi hii kila siku na maisha yako yatakuwa bora sana.
Ukawe na wakati mwema na maandalizi mema ya siku ya kesho, ikawe siku ya upendo mkubwa kwako, ujipende mwenyewe, uwapende wanaokuzunguka na upende kile unachofanya.
Kocha.