Do not regret the past. What is the use of regrets? The lie says that you should regret. The truth says you should be filled with love. Push all sad memories away from you. Do not speak of the past. Live in the light of love, and all things will be given to you. —PERSIAN WISDOM
Ni siki nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Usijutie mambo yaliyopita, kwa sababu majuto hayana faida yoyote.
Uongo unasema unapaswa kujutia mambo yaliyopita.
Ukweli unasema unapaswa kuishi kwa upendo.
Weka kumbukumbu zote pembeni, usizungimzie yale yaliyopita.
Badala yake ishi kwenye wakati uliopo, ishi kwa upendo na kila kitu utapewa.
Haijalishi ni makosa au mambo mabaya kiasi gani umeyafanya siku za nyuma, kuyajutia leo haitakuwa na msaada wowote kwako.
Badala yake chagua kuishi kwenye wakati ulionao sasa,
Kuishi kwenye wakati huo kwa upendo,
Kufanya kile ambacho ni sahihi kufanya.
Wakati uliopo ndiyo wakati pekee ulionao kwenye maisha yako,
Usikubali kuupoteza kwa kujutia yale ambayo yameshapita.
Ishi sasa, ishi kwa upendo na fanya kilicho sahihi.
Uwe na siku bora leo, siku ya kuishi wakati ulionao na kutoruhusu majuto yakutawale.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania