“Your purpose in life is to find your purpose and give your whole heart and soul to it.” – Buddha

Kusudi kuu la maisha yako ni kulijua kusudi la maisha yako na kisha kuweka juhudi zako zote katika kufikia kusudi hilo.
Jua umekuja hapa duniani kufanya nini kisha kifanye kila siku.
Weka kazi, kazana kuwa bora zaidi na toa thamani kwa wengine.

Kama bado hujalijua kusudi lako, unachofanya ni kuwasindikiza wengine,
Na hao wengine watakutumia katika kufikia kusudi la maisha yao.
Unapolijua kusudi la maisha yako na hilo likawa ndiyo kazi yako kuu,
Hakuna tofauti kati ya maisha na kazi,
Hakuna tofauti kati ya kazi na kucheza,
Unakuwa mmoja na kila unachokifanya ni kwa umoja wa akili, mwili na roho.

Uwe na usiku mwema, usiku wa kujiandaa vyema ili kwenda kuliishi kusudi lako kesho.
Kocha Dr Makirita Amani,