This world, only this world, is the place of our work, and all our forces, all our efforts, should be directed toward this life. – Leo Tolstoy

Kwenye hii dunia ndiyo sehemu pekee unayoweza kuonesha kazi yako,
Hivyo peleka nguvu zako zote kwenye kila unachofanya.
Hutapata nafasi nyingine ya kufanya kazi zako, hivyo zifanye sasa.
Huna uhakika wa kupata siku nyingine ya kuweza kufanya kazi zako, hivyo zifanye leo.

Usipoteze muda wako kwa mambo mengine yasiyo na manufaa kwako,
Fanya kazi zako, kwa juhudi na upekee,
Na hakuna kazi inayoenda bure, kila unachofanya, dunia itakulipa.
Nenda kaweke kazi leo, hilo ndiyo la muhimu.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania