“In the life of a man, his time is but a moment, his being an incessant flux, his body a prey for worms, his fortune dark and his fame doubtful. In short, life is a brief sojourning in an alien land. And after this, oblivion.” – Marcus Aurelius
Maisha yetu wanadamu ni mafupi mno ukilinganisha na umri ambao dunia imekuwepo.
Maisha hayo ni kama nukta, leo upo na kesho haupo.
Mbaya zaidi hujui ni kesho ipi ambayo hutakuwepo.
Hivyo yatupasa kuwa tayari wakati wote.
Mambo mengi yanayokusumbua sasa, hayatakuwa na maana utakapoondoka.
Mengi yatasahaulika mara tu utakapoondoka.
Mwili wako utakuwa chakula cha wadudu.
Lakini kuna vitu vinavyoweza kubaki hata baada ya kuwa umeondoka.
Kimoja wapo ni jinsi unavyogusa maisha ya wengine kwa namna ya kipekee na kuyafanya kuwa bora zaidi.
Kwa kuwa na upendo, kujali, kutenda wema na kujitoa kwa ajili ya wengine, unaacha alama bora kwao.
Kingine ni kitu ulichozalisha kwa mikono yako na chenye manufaa kwa wengine.
Kwa kuandika kitabu, kupanda miti, kusanifu majengo na mengine yatabaki na watu hata baada ya kuondoka.
Hivyo kila zawadi ya siku mpya tunayoipata, swali muhimu kujiuliza ni NINASUMBUKA NA NINI.
Je unasumbuka kutumia muda wako mfupi kwa mambo ambayo yatasahaulika muda mfupi baada ya kuondoka?
Au unasumbuka na yale yatakayoacha alama.
Majibu unayo mwenyewe, muhimu ni usijidanganye.
Hakuna atakayekumbukwa kwa habari alizofuatilia, mitandao aliyotumia, starehe alizoendekeza na malalamiko aliyokuwa anatoa.
Kuendekeza mambo hayo ni kuchagua kupoteza muda wa thamani ulionao.
Usikubali kufanya hivyo, tumia muda wako vyema, tambua mengi yanayokusumbua yatapotea kama moshi utakapokufa, hivyo amua kuyapoteza sasa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu vigezo vya kuzingatia kwenye kazi au biashara utakayofanya kwa muda mrefu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/18/2057
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.