
Utapeli huwa hautofautiani sana, ukiwa na akili kidogo tu na ukaitumia, utaona wazi viashiria vya utapeli.
Na matapeli wanajua kuna viashiria vilivyo wazi na pale unapouliza kuhusu hilo tayari wana majibu.
Watakuambia hii ni tofauti na nyingine ambazo utakuwa umefananisha nazo.
Na kama utaendelea kuuliza zaidi watakuonesha wengine ambao tayari wananufaika, ili wivu ukuingie, uone unapitwa kama hutaamua na usukumwe kuamua haraka.
Matapeli wanahitaji vitu viwili ili wakunase, hisia zako kuwa juu na kukuharakisha kufanya maamuzi.
Epuka saba kauli hizo za hii ni tofauti na wenzako wananufaika, jipe muda wa kuitafakari kila fursa kabla hujaingia.
Na unapokuwa na wasiwasi juu ya fursa fulani na majibu unayopewa ni hayo ya kwamba ni tofauti na nyingine au wengine wananufaika, basi jua wasiwasi wako ni sahihi na epuka sana fursa hiyo.
Ukurasa wa kusoma ni kuchezea mfumo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/11/2293
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma