
Kama watu wanakulalamikia kwamba hueleweki, hawayaelewi maisha yako hilo lisikusumbue sana. Maana hakuna yeyote anayeiona dunia kwa namna unavyoiona wewe.
Imani, mtazamo, fikra na uzoefu ulionao ni wa kipekee, ukiishi kwa kuzingatia hayo, utakuwa tofauti kabisa na wengine.
Na kuwa tofauti haimaanishi unakosea, bali inamaanisha unafanya kilicho sahihi kwako.
Watu wakikuambia hawakuelewi maana yake hawajapata namna ya kukudhibiti, kitu ambacho ni kizuri kwa sababu unakuwa huru zaidi.
Hakuna anayeweza kukuelewa na wala huwezi kuwaelewa wengine, hivyo weka juhudi zako kwenye kuyaishi maisha yako na waache wengine nao wayaishi maisha yao.
Ukurasa wa kusoma ni u mpweke; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/29/2311
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma