
Kama watu wanakufanyia vitu ambavyo vinakuudhi ni kwa sababu labda hawajui kama vitu hivyo vinakuudhi au wanafanya makusudi. Lakini kwa sehemu kubwa wanakuwa hawajui.
Na wewe huwaambii, unategemea wawe wanajua wenyewe, kitu ambacho hakitokei.
Chochote unachotaka watu wajue kuhusu wewe, waambie wewe mwenyewe. Ili wanapofanya tofauti na unavyotaka, ujue wazi wamefanya wakiwa wanajua.
Watu hawawezi kusoma mawazo yako na kujua nini unataka. Sema wazi unachotaka, eleza wazi unachosimia, hilo linaweza kuwaumiza baadhi, lakini litawafanya waheshimu kile unachotaka.
Ukurasa wa kusoma ni kutokuyazungusha maisha; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/09/2321
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma