Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ulichosomea.
Tatizo kubwa la mfumo wa elimu unaotumika sasa ni kuwaandaa wanafunzi kwa njia moja tu ya kuingiza kipato, kuajiriwa.
Wanafunzi wanafanya vizuri na kuhitimu, lakini nafasi za ajira hakuna.
Kinachotokea ni wengi kukata tamaa na kuona elimu waliyopata haina maana.
Elimu yoyote uliyopata unaweza kuitumia kuingiza fedha kwa njia mbalimbali. Hapa tunakwenda kushirikishana njia kumi za kufanya hivyo.
- Iliyo maarufu zaidi, kuajiriwa.
-
Kuwa mshauri elekezi (consultant) kwenye eneo ulilosomea.
-
Kuandika kitabu kinachoendana na uliyosomea kuwalenga watu wa kawaida.
-
Kufanya biashara inayoendana na ulichosomea.
-
Kuandaa kozi ya mafunzo yenye manufaa kwa wenye uhitaji au matatizo kwenye eneo ulilosomea.
-
Kuhamishia ujuzi na uzoefu uliopata kwenye ulichosomea na kupeleka kwenye kitu kingine ili uweze kukifanya kwa tofauti.
-
Kuwa mtu wa kati unayewaunganisha walio kwenye tasnia uliyosomea na wale ambao wanahitaji vitu fulani ila hawajui jinsi ya kuvipata.
-
Kuanzisha chuo cha kuwafundisha wengine kile ulichosomea.
-
Kutafiti na kuandika kitabu cha kitaaluma kwenye tasnia uliyosomea.
-
Kujiajiri au kufanya biashara ya tofauti na ulichosomea ila kutumia ujuzi na uzoefu wa ulichosomea kujitofautisha na kufanya kwa ubora.
Kwa kufungua fikra zako na kuangalia kile ulichosomea utaziona fursa hizi na nyingine na mahali pa kuanzia ili uweze kupiga hatua.
Usidharau ulichosomea na kuona hakina manufaa.
Kocha.