Usisubiri mpaka upate hamasa ndiyo uanze kufanya kile unachotaka kufanya. Badala yake anza kukifanya na utatengeneza hamasa ya kuendelea kukifanya zaidi.

Ukisubiri mpaka upate hamasa ndiyo uanze utajichelewesha. Ukianza kabla hata hujawa na hamasa unajenga hamasa ya kuendelea kufanya.

Kama ilivyo kanuni ya sayansi, kilichosimama huendelea kusimama wakati kilicho kwenye mwendo huendelea na mwendo.

Wewe usisimame, anzisha mwendo na endelea nao.

Ukurasa wa kusoma ni mtazamo na matendo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/24/2336

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma