Msongo wa mawazo unaosababishwa na matumizi ya mitandao ya kijamii ni wa kujitakia.

Unajiweka mwenyewe kwenye mazingira ambayo watu wengi unaojihusisha nao huwajui halafu unakazana kujilinganisha nao wakati kila mmoja anaishi maisha ya maigizo huko mitandaoni.

Unaweza kujionea mwenyewe kwa nini lazima upate msongo kwenye mitandao hiyo usipokuwa makini.

Ni bora utumie muda wako kujenga na kuimarisha mahusiano yako na wale unaowajua moja kwa moja kuliko kuhangaika na ya mtandaoni.

Ukurasa wa kusoma ni mageuzi ya teknolojia kupiku mageuzi ya akili; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/02/2345

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma