Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa nguo za mitumba.
Mavazi ni hitaji la msingi kabisa la watu. Lakini siyo wote wanaoweza kumudu kununua nguo ambazo ni mpya.
Hasa ukizingatia ubora na matumizi, kwa wengi nguo za mitumba zinawafaa zaidi kuliko ambazo ni mpya kabisa.
Hili linafungua fursa ya mtu kuweza kuingiza fedha kwa biashara ya nguo za mitumba.
Hapa ni mawazo 10 ya kuweza kufanya hivyo.
- Kununua nguo za mtumba kwa jumla na kuuza kwa reja reja.
-
Kuuza kwa kutembea maeneo yenye magulio.
-
Kuwa na timu ya wauzaji ambao wanaenda sehemu mbalimbali.
-
Kuagiza mzigo mkubwa wa mitumba na kuuza kwa jumla.
-
Kutumia mitumba kupata vitambaa vya kutengeneza vitu vingine kama mikoba.
-
Kutafuta masoko kwa wauzaji wa nguo za mitumba.
-
Kujua jinsi ya kuchagua mzigo mzuri na unaopendwa na wateja.
-
Kujua mahitaji ya masoko mbalimbali na kujua soko lipi la kupeleka aina ya mzigo uliopata.
-
Kutumia mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii kuuza zaidi.
-
Kutengeneza wateja wanaokutegemea kwenye kununua nguo hizo za mtumba.
Unapofanya biashara hii, unajifunza mengi sana ukiwa ndani na kuziona fursa za kufanya kwa ubora zaidi.
Kocha.
Asante sana kocha kwa hili
LikeLike
Karibu Godius.
LikeLike