
Ukiwa na furaha utajua, huhitaji kujiuliza mara mbilimbili kama una furaha au la. Ukifanikiwa utajua, huhitaji kujihoji kama umefanikiwa.
Mambo yote muhimu kwenye maisha, unayajua wazi kama unayo au la na kama bado unajiuliza, basi jibu ni huna.
Tafakari ni maswali gani umekuwa unajiuliza mara kwa mara, jua nini unakosa mpaka ujiulize maswali hayo na tatua ulichokosa.
Ukurasa wa kusoma ni kama bado unajiuliza jibu ni hapana; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/18/2361
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma