Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mauzo.
Kama kuna watu wamefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa duniani basi ni watu wa mauzo.
Wagunduzi mbalimbali waliweza kugundua vitu vizuri, lakini ni watu wa mauzo ndiyo walioweza kuwashawishi watu wakubali kununua vitu hivyo.
Kwa kuwa watu wana mahitaji mbalimbali, sehemu ya mauzo ni muhimu na inatoa fursa kwa yeyote mwenye kuweza kuelewa kitu na kujenga ushawishi kuweza kuingiza kipato.
Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza fedha kupitia mauzo.
- Kuwa mtu wa mauzo kwa bidhaa au huduma yako mwenyewe na kuweza kuuza zaidi.
-
Kuajiriwa kama mtu wa mauzo kwenye kampuni au taasisi mbalimbali.
-
Kuwa mtu wa mauzo kwa kamisheni kwa kampuni na taasisi mbalimbali ambapo unalipwa kulingana na mauzo uliyofanya.
-
Kutengeneza mfumo mzuri wa mauzo na kuuza kwa kampuni na taasisi mbalimbali.
-
Kufundisha wengine mfumo mzuri wa mauzo na wakalipa kupata mafunzo hayo.
-
Kuandika makala na vitabu kwenye eneo la mauzo na watu wakanunua.
-
Kutumia mitandao ya kijamii kujenga jukwaa la mauzo ambalo unaweza kulitumia kuuza vitu mbalimbali.
-
Kuwa mtu wa mauzo unayetembea maeneo mbalimbali na hivyo kuteka soko kubwa.
-
Kuwa mshauri elekezi kwenye mauzo hasa ya bidhaa au huduma mpya ambayo soko haijajua.
-
Kufanya tafiti mbalimbali za mauzo na kuuza matokeo kwa kampuni au taasisi zinazotaka kukuza mauzo yake zaidi.
Eneo la mauzo ni eneo ambalo halihitaji upendeleo wowote ndiyo upewe nafasi.
Unachohitaji ni kuonyesha kwa vitendo kwamba unaweza kuuza na watu watakua tayari uwasaidie kuuza bidhaa na huduma zao na wakulipe vizuri.
Kwa kuanza na njia hizi kumi, unaweza kutengeneza kipato kizuri kupitia mauzo.
Kocha.