Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kuuza nguo mtandaoni.
Mavazi ni mahitaji ya msingi ya watu.
Kwa zama tunazoishi sasa, huhitaji kuwa na duka ndiyo uweze kuingia kwenye biashara hii.
Unaweza kuuza kwa njia ya mtandao na kutengeneza kipato.
Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza fedha kwa kuuza nguo mtandaoni.
- Kuwa na blog ambayo inakuwa ndiyo duka lako la mtandaoni, unaweka picha za nguo na maelezo mafupi.
-
Kuwa na ukurasa kwenye mtandao wa facebook ambapo unaweka picha za nguo na maelezo mafupi.
-
Kuwa na ukurasa kwenye mtandao wa instagram ambapo unaweka matangazo ya nguo.
-
Kulipia matangazo kwenye mitandao ya kijamii na kuchagua aina ya watu ambao unataka yawafikie, hapo unawafikia wengi kwa pamoja.
-
Kutengeneza na kutunza taarifa za wateja tarajiwa na wateja halisi ili kuendelea kuwasiliana nao.
-
Kutengeneza kundi la wasap ambapo utawashawishi wateja kujiunga ili kupata taarifa za mapema.
-
Kuwa na mfumo wa kutuma ujumbe mfupi wa moja kwa moja kwa wateja ili kuwa na ushawishi zaidi.
-
Kuwapa wateja zawadi pale wanapoleta wateja wengine.
-
Kuendesha mashindano mbalimbali ambapo wateja wanasambaza taarifa kwa wengi zaidi ili kuweza kushinda zawadi.
-
Kuwa na channel ya YouTube ambapo unaweka video zinazohusu mambo ya mavazi, ukawashawishi watu kununua lakini pia ukaingiza kipato kwa matangazo mengine.
Kocha.