Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ushereheshaji.

Watu huwa wanafanya matukio mbalimbali kwenye maisha na kuhitaji washereheshaji (MC) wa kuyaendesha matukio hayo.
Hili linatoa fursa kwa mtu kuweza kuingiza kipato kama mshereheshaji.

Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia ushereheshaji;

  1. Kuendesha shughuli za sherehe kwa watu binafsi.

  2. Kuendesha mikutano ya makampuni na taasisi mbalimbali.

  3. Kutengeneza matangazo mbalimbali ya sauti na video.

  4. Kuwafundisha wengine ushereheshaji.

  5. Kutumia mitandao ya kijamii kupata wateja zaidi.

  6. Kuandika vitabu na kutoa maarifa kuhusu ushereheshaji.

  7. Kuwa balozi wa kampuni au taasisi mbalimbali.

  8. Kuwa msemaji wa kampuni au taasisi mbalimbali.

  9. Kuandaa makongamano mbalimbali.

  10. Kutumia kazi zako za ushereheshaji na mtandao wako wa uliowahi kufanya nao kazi ili kupata kazi zaidi.

Kama unaweza kujieleza vizuri mbele za wengine, wakakuelewa na kushawishika, una fursa nyingi mbele yako kama mshereheshaji. Jiendeleze kwenye eneo hilo na uzitumie fursa zilizopo.

Kocha.