Adui mkubwa wa mafanikio na maendeleo ni kuridhika na kile ambacho mtu ameshapata.

Ugunduzi na hatua zote ambazo tumepiga kama wanadamu, ni kwa sababu watu hawakuridhika na kile walichokuwa nacho, japo kilikuwa bora.

Iphone ya kwanza kutengenezwa yalikuwa mapinduzi makubwa mno, kila mtu alipenda namna teknolojia ilivyopiga hatua. Leo kuna iphone ya 12 ambayo ukilinganisha na ya kwanza, utaona ya kwanza siyo kitu kabisa.

Kitu chochote kile, kinaweza kufanywa kwa ukubwa na ubora zaidi ya kilivyo sasa.

Hivyo usiridhike na kubweteka na kile unachofanya sasa au pale ulipofika. Badala yake pambana kufanya kwa ukubwa na ubora zaidi, hiyo ndiyo njia ya kufanikiwa zaidi.

Kila wakati jiulize namna gani unaweza kufanya kwa ukubwa na ubora zaidi? Kisha chukua hatua ili usibaki hapo ulipo sasa.

Dunia inaenda kasi sana, kuridhika na kubaki pale ulipo ni kuchagua kurudi nyuma, usikubali hilo.

Kutokuridhika haimaanishi kwamba unajiona hujakamilika, bali unaona fursa za kufanya kwa ubora zaidi.

Ukurasa wa kusoma ni kubwa na bora; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/28/2371

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma