Kama kitu kimezaliwa au kuanzishwa, kinapaswa kukua.

Kama hakuna ukuaji maana yakr kuna tatizo, kuna kikwazo kinachozuia kitu hicho kisikue.

Wajibu wako ni kujua tatizo au kikwazo kiko wapi, kukifanyia kazi ili kitu kiweze kukua.

Na ili ujue kama kitu kinakua au la, lazima uwe na njia ya kukipima.

Bila kupima utajidanganya mambo yako vizuri wakati siyo. Kila unachoanzisha, kifuatilie ka karibu na uhakikishe kinakua zaidi.

Ukurasa wa kusoma ni vinavyozuia biashara kukua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/03/2376

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma