Sababu nyingi unazojipa za kwa nini hujaweza kufanya au kupata unachotaka siyo sababu halisi, bali ni visingizio tu.

Kwa visingizio hivyo umekuwa unajidanganya na kujifariji, kitu ambacho ni kikwazo kwa mafanikio yako.

Kama kuna kitu unajipa kama sababu ya kikwazo, lakini wengine wameweza kuvuka kitu hicho, basi hiyo siyo sababu, bali ni kisingizio tu.

Kwani hao wengine wameweza wana nini na wewe ushindwe una nini? Ona aibu kutoa sababu ambazo wengine wamezivuka.

Achana na hivyo visingizio na weka juhudi mpaka upate kile unachotaka.

Ukurasa wa kusoma ni sababu na visingizio; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/11/2384

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma