#SheriaYaLeo (5/366); Jua kinachokuvutia na zama ndani.

Kama umefanyia kazi sheria 4 zilizopita, utakuwa umeshajua ni kitu au vitu gani unavyovutiwa sana kuvifanya.

Vitu vinavyotokana na sauti yako ya ndani, ambavyo huchoki kuvifanya na upo tayari kuvifanya bila kujali wengine wanasema au kufanua nini.

Hivyo ndiyo vitu ambavyo vinatoka ndani yako kweli, vinatokana na kusudi na wito wako hapa duniani.

Kinachofuata ni wewe kuzama ndani kwenye kuvifanya vitu hivyo. Vifanye kwa kina hasa, kwa kuhakikisha unafanya kwa umakini na viwango vya juu.
Hakikisha unavijua vitu hivyo nje ndani na kwa kila namna.

Ni kupitia kuzama ndani kwenye kufanya vitu vinavyokuvutia sana ndiyo unaweza kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti, ambayo yanaacha alama kubwa pia.

Sheria ya leo; Ni kitu gani umekuwa unavutiwa sana kukifanya kwa muda mrefu? Zama ndani kwenye kukifanya kitu hicho leo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma