#SheriaYaLeo (191/366); Wafanye wengine wajipendekeze kwako.
Ili kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu, wanatakiwa wawe wanakuhitaji wewe zaidi ya unavyowahitaji wao.
Hivyo unapaswa kutengeneza hali itakayowafanya wengine wakuhitaji zaidi na hilo litawafanya wajipendekeze kwako.
Njia ya kwanza ya kufanya hivyo ni kuwa na uhuru kamili na wenye nguvu. Kutokutegemea chochote au yeyote. Hali hiyo ya uhuru kamili inawafanya wengi kuvutwa kuja kwako.
Wakati wale wenye utegemezi mkubwa kwa wengine wakionekana kama mzigo.
Njia nyingine ni kuwa na matakwa makubwa kutoka kwa wengine na kutokuhofia kutaka kile unachotaka.
Watu huwaheshimu wale wanaojua wanachotaka na wamejitoa kweli kuhakikisha wanakipata.
Wakati wale wanaohofia kwenye kile wanachotaka wakidharauliwa.
Kuwa huru na simamia kile unachotaka na wengine watavutwa zaidi kuja kwako, huku wakiwa tayari kukupa unachotaka.
Sheria ya leo; Uhuru kamili unawafanya wengine watutegemee kwa kiasi kikubwa. Hilo linawafanya wawe tayari kutupa kile tunachotaka. Kuwa huru na simamia unachotaka bila ya kuhofia chochote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji