#SheriaYaLeo (192/366); Tengeneza habari inayosambaa.
Pale watu wanapojua kuna kitu unataka, iwe ni kura, kuuza au kukubalika, wanaleta ukinzani.
Wanaibuka watu ambao watakupinga kwenye kile ambacho unakitaka.
Kuepuka hilo, unapaswa kuficha nia yako nyuma ya tukio ambalo litakuwa habari inayosambaa kwa wengi.
Habari hiyo inayosambaa inakamilisha nia yako bila ya kuonekana wazi kile unachotaka.
Ili habari unayotengeneza iweze kusambaa kwa wengi, inapaswa kuwa tofauti kabisa na habari nyingine zilizopo.
Linapaswa kuwa tukio ambalo kila chombo cha habari kinakimbilia kuliripoti na watu wanataka kulifuatilia ili wasipitwe na kinachoendelea.
Ni muhimu ulipe tukio hilo uhusiano chanya ili watu wawe tayari kwenda nalo.
Lifanye kuwa tukio la kizalendo, kijamii au kiroho kwa namna ambayo wengi wanaguswa nalo.
Kwa njia hiyo, watu watajishawishi wenyewe kujiunga kwenye mkumbo wa habari hiyo inayosambaa.
Na hapo zoezi la ushawishi kwao linakuwa rahisi na hutengenezi upinzani.
Hakuna anayependa kupitwa na yale yanayoendelea.
Unapotengeneza habari inayosambaa kwa kasi, wengi wanajiunga nayo wao wenyewe na hapo kuwa tayari wameshawishika.
Sheria ya leo; Onekana kuwa nyuma ya kila matukio na habari zinazosambaa kwa wengi na watu watakimbilia kujiunga na wewe ili wasiachwe nyuma. Kwa njia hiyo ushawishi unakuwa rahisi bila ya upinzani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji