#SheriaYaLeo (193/366); Kutoka urafiki kuwa wapenzi.
Kutoka kwenye urafiki mpaka kuwa wapenzi ni kitu kinachoweza kutokea kwa ushawishi usio wa moja kwa moja.
Kwanza unaanza kwa mazungumzo ya kirafiki na yule unayemlenga. Mazungumzo hayo yanakupa fursa ya kumjua kiundani, kujua tabia zake, madhaifu yake na yale anayotaka sana.
Mbili kwa kutumia muda mwingi na unayemlenga inamfanya akuzoee na kujisikia vizuri pale anapokuwa na wewe.
Hapo anaamini unakubali mawazo yake na kupenda uwepo wake.
Hilo linaondoa hali ya ukinzani na kumfanya kuwa rahisi kushawishika pale unapotaka zaidi.
Urafiki huo unakuwa umefungua mlango wa ushawishi kwenye fikra zako.
Chochote utakachosema au kufanya kitapokelewa vizuri.
Hilo litamfanya mtu kuwa na hisia kwamba kuna kitu cha zaidi baina yenu.
Na hapo inakuwa rahisi kumshawishi kuwa wapenzi, kwani anaona ni kama yeye ndiyo anafanya hivyo.
Kwa kuanza na urafiki, kujali kuhusu mtu na kumwelewa kwa undani kunajenga ushawishi mkubwa ambao unarahisisha kwenda hatua ya wapenzi.
Sheria ya leo; Anza kwa kutengeneza urafiki wa kawaida, kisha kusogea kidogo kidogo kutoka urafiki kwenda wapenzi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji