#SheriaYaLeo (201/366); Wanase kwenye dunia ya ndoto yako.
Watoto huwa wana uwezo wa kutengeneza dunia ya ndoto yao na kuishi kwenye dunia hiyo kifikra.
Bila ya kujali nini kinaendelea nje, ndani yao wanajiona wakiwa kwenye dunia wanayoitaka.
Hiki siyo kitu kinachowafaa watoto pekee, bali hata watu wazima kinawafaa sana.
Unaweza kutengeneza dunia ya ndoto yako kwenye fikra zako na kuishi kwenye dunia hiyo kifikra.
Unapokuwa na dunia ya aina hiyo, usikubali kuiacha, badala yake unapaswa kuwanasa wengine waingie kwenye dunia yako.
Kwa kuwa wengi hawana uthubutu wa kujenga dunia za ndoto zao na kuishi humo, watavutiwa na kushawishika na wewe ambaye umejenga dunia ya ndoto yako na unaishi humo kwa msimamo.
Dunia ya kutengeneza kifikra ni tofauti na dunia halisi.
Ni dunia inavyokuwa vile mtu anavyotaka na hivyo kuweza kuifurahia.
Watu huvutiwa kwa wale wanaoyafurahia maisha yao.
Hivyo kwa kutengeneza dunia ya ndoto yako na kuifurahia, utawanasa wengi kuja kwako na kuwa na ushawishi mkubwa kwao.
Sheria ya leo; Jifunze kucheza na taswira yako, kamwe usiichukulie kwa uzito sana. Jenga dunia ya ndoto yako kwenye fikra zako na ishi kwenye dunia hiyo kwa msimamo. Kadiri unavyokuwa umezama kwenye dunia yako, ndivyo wengi wanavyovutiwa kwako na kushawishika na wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji