#SheriaYaLeo (253/366); Ona hatari kubwa iliyo mbele yako.

Changamoto kubwa ambayo watu wengi wanayo ni kunasa kwenye wakati uliopo na kushindwa kabisa kupangilia yale yanayokuja.

Matokeo yake ni mambo yanakuja kwao kwa mshangao mkubwa, wakiwa hawana maandalizi yoyote, kitu ambacho kinawaathiri sana.

Wewe usiwe kama walio wengi, usikubali kuvurugwa na yale yanayoendelea sasa.
Badala yake angalia makubwa yanayokuja na yapangilie.
Kuwa na mpango wa mambo makubwa ya mbeleni na fanyia kazi mpango wako.

Kwa kuweza kupangilia makubwa yajayo na kuziona hatari kubwa zinazoweza kuja kabla hujazifikia, unakuwa na maandalizi bora ya kuweza kukabiliana na chochote.
Hilo linakupa mamlaka makubwa na kukuwezesha kutoa matokeo makubwa na ya tofauti.

Sheria ya leo; Yavuke mazoea ya binadamu ya kunasa kwenye wakati uliopo. Badala yake jifunze kuangalia makubwa yanayokuja na kuwa na maandalizi ya kuweza kuyakabili. Usikubali chochote kikukute kwa mshangao.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji