#SheriaYaLeo (254/366); Puuza mambo kuyanyima nguvu.
Jambo lolote lile huwa linakuwa na nguvu kwetu pale tunapolijali na kulipa umakini wetu.
Hata watu huwa wanatusumbua kwenye mambo ambayo tunayajali sana.
Lakini unapopuuza jambo lolote lile, unalinyima nguvu na hivyo halikusumbui.
Hata watu wanapotaka kukusumbua, ukiwapuuza usumbufu wao unakosa nguvu kwako.
Kupuuza ni kitu chenye nguvu na kinachokupa wewe mamlaka makubwa.
Kamwe usikubali kuonyesha kwamba kitu kimekuathiri au ni muhimu zaidi kwako.
Chochote ambacho hutaki kikusumbue basi kipuuze.
Sheria ya leo; Kwa kulitambua tatizo dogo unalipa nguvu ya kukusumbua na hata kulikuza. Njia ya uhakika ya kunyima chochote nguvu ni kukipuuza, inakupa wewe mamlaka makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji