#SheriaYaLeo (256/366); Muda ndiyo kitu pekee ulichonacho.
Muda ni rasilimali muhimu sana uliyonayo kwenye maisha yako.
Kuweza kutumia muda wako vizuri kunakufanya uweze kufanya makubwa zaidi.
Ili kuweza kunufaika vizuri na muda, lazima uuchukulie kwa tofauti na ambavyo umekuwa unauchukulia.
Kiuhalisia, tangu siku uliyozaliwa, muda ndiyo kitu pekee ulichonacho.
Ndiyo rasilimali kuu ambayo una umiliki nayo mkubwa.
Watu wanaweza kuchukua rasilimali zako nyingine, lakini kwenye muda, kama wasipokuua, hawawezi kuchukua muda wako.
Hata mtu mwenye mamlaka makubwa duniani, hawezi kuchukua muda wako kama hujamruhusu.
Hata kama utakuwa umefungwa gerezani, bado muda wako uko kwenye umiliki wako na unaweza kuutumia vile unavyotaka wewe.
Kupoteza muda kwenye mambo yasiyokuwa na tija siyo tu makosa, bali ni upumbavu wa hali ya juu.
Usipoteze rasilimali kuu uliyonayo, ambayo ndiyo maisha yako.
Badala yake itumie kwa manufaa kwako.
Sheria ya leo; Jizue kuhangaika na mambo yasiyokuwa na tija. Ukishapoteza muda huwezi kuupata tena. Tumia muda wako kwa mambo yenye tija pekee.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji