#SheriaYaLeo (292/366); Fikiria kama mwandishi.
Waandishi huwa wanachunguza kitu kwa ndani ili kuweza kujua uhalisia wake.
Huwa hawachukulii kitu juu juu kama wanavyofanya watu wengine.
Kwanza kabisa wanajizuia wasihukumu kitu chochote kile wanachofanya watu, hata kama ni kibaya kiasi gani.
Huchukulia kwamba watu wana sababu ya kila wanachofanya, sababu inayoonekana ni sawa kwao.
Hata wale ambao wanafanya mambo ya hovyo kabisa, ndani yao wana sababu nzuri za kufanya hivyo.
Na wengi wanakuwa wana maumivu makubwa ndani yao kutokana na yale waliyopitia.
Ni kwa njia hiyo ndiyo huwa wanaweza kuwaelewa watu kwa kina na hata kuweza kuwasamehe kwa yale wanayofanya.
Hivyo ndivyo unavyopaswa kufikiri na kuwachukulia watu.
Badala ya kukimbilia kuwahukumu, waelewe kwa kina na utaona wanastahili huruma badala ya hukumu.
Sheria ya leo; Fikiria kama mwandishi katika kuwakabili watu unaojihusisha nao, hata wale unaowaona ni wabaya kabisa. Wana sababu za kuwa wanavyokuwa na unapozijua utawaonea huruma badala ya kuwahukumu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji