#SheriaYaLeo (294/366); Ona zaidi ya wakati uliopo.

Sisi binadamu huwa tuna tabia ya kuishi kwenye wakati uliopo.
Hii ni sehemu kubwa ya asili yetu, ambayo tumeipata kutoka kwa wanyama.

Mara nyingi huwa tunakimbilia kujibu kile kilicho mbele yetu kwa wakati husika, ambacho kinanasa umakini wetu zaidi.

Lakini sisi siyo tu wanyama ambao tumenasa kwenye wakati uliopo.
Asili ya binadamu inahusisha wakati uliopota, uliopo na ujao.
Mambo yote yanayoendelea kwenye maisha yetu, mzizi wake upo kwenye wakati uliopita.

Kila tatizo unalopitia sasa, limeungana na mambo mengi yaliyopita pamoja na kuathiri mambo yajayo.
Chochote tunachofanya, kina madhara ambayo ni ya muda mrefu ujao.

Pale tunapofanya maamuzi kwa kutumia wakati uliopo pekee, tunajishusha kwenye ngazi ya wanyama ambao hufanya maamuzi bila kufikiri.
Hisia na tamaa tunazokuwa nazo kwenye wakati husika ndiyo zinaamua aina ya maamuzi ambayo mtu utafanya.

Matapeli na watu wanaotaka kutulaghai huwa wanatumia sana njia hiyo kuwasukuma watu kufanya maamuzi kwa kutumia wakati uliopo na kusahau uliopita na ujao.
Wanapokupa fursa yenye manufaa kwenye wakati ujao, unasahau kuuliza kuhusu wakati uliopita na hata ujao.

Manufaa ya haraka yanatuhadaa na kutupumbaza kwa kuingiwa na tamaa.
Tunashindwa kuzingatia mambo ya msingi kuhusu yaliyopita na yajayo na hilo kupelekea kufanya maamuzi mabovu kwetu.

Njia pekee ya kujikinga na hilo ni kujifunza kuacha kutumia wakati uliopo pekee.
Badala yake tunapaswa kuangalia yaliyopita na yajayo ili kuweza kuwa na mtazamo sahihi wa kutuwezesha kufanya maamuzi sahihi.
Unapaswa kuepuka tamaa ya wakati uliopo na kuangalia mambo ya aina hiyo huko nyuma yaliishia wapi.
Pia kujua kila hatua unayochukua sasa, inatengeneza mambo mengi ya mbele, hivyo unapswa kuchukua hatua kwa tahadhari.

Sheria ya leo; Badala tu ya kunasa kihisia kwenye jambo lililo mbele yako, unapaswa kwenda mbele na nyuma kabla ya kufanya maamuzi.
Zingatia historia ya kitu husika huko nyuma na madhara ya muda mrefu ya kila hatua unayoweza kuchukua sasa.
Ni kwa njia hiyo ndiyo unaweza kufanya maamuzi bora.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji