#SheriaYaLeo (295/366); Tambua msukumo wako wa shari.
Sisi binadamu tuna asili ya ushari.
Na hilo siyo jambo baya mara zote.
Maana ni ushari huo ndiyo unaotupa msukumo wa kufanya makubwa na kufanikiwa.
Lakini pale ushari huo unaposhindwa kudhibitiwa vizuri, unakuwa chanzo cha machafuko makubwa.
Wizi, utapeli, uhasama na vita yote ni matokeo ya ushari ambao haujadhibitiwa vizuri.
Tambua msukumo wa ushari ambao upo ndani yako na uelekeze huo kwenye mambo yenye manufaa kwako na kwa wengine.
Peleka shari yako kwenye kupambana na umasikini au changamoto nyingine zinazokukabili wewe au wengine.
Kwa kufanya kilicho sahihi na kisichowaumiza wengine.
Msukumo wa shari ukitumika vizuri, utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Sheria ya leo; Angalia dalili za msukumo wa shari kwako binafsi kwenye mambo yaliyopita. Ona ni jinsi gani msukumo huo ulipelekea kupata mafanikio au kuleta misuguano na wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji