2794; Ni muda.
Warren Buffett amewahi kusema huwezi kupata mtoto ndani ya mwezi mmoja kwa kuigawa mimba moja kwa wanawake 9.
Wote tunajua mimba huwa inachukua miezi tisa kwa mtoto kukamilika na kuzaliwa.
Sasa miezi hiyo tisa ni ya kujikusanya pamoja.
Huwezi kuigawa kwa wanawake 9 kama njia ya mkato ya kupata mtoto haraka.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye safari ya mafanikio.
Muda ni kipengele muhimu ambacho hakuna namna unaweza kukibadili.
Unaweza kuweka juhudi kubwa uwezavyo.
Unaweza kujifunza mapya na kuyajaribu.
Na unaweza kufanya kupitiliza.
Lakini swala la muda huwezi kuliathiri.
Bado huwezi kuharakisha muda kuliko ilivyo kawaida.
Hivyo kama tayari unaweka juhudi sahihi.
Kama unaendelea kujifunza na kuwa bora.
Lakini nado huyaoni matokeo uliyoyatarajia.
Usikate tamaa, jua muda ndiyo bado.
Wewe uendelea kukaa kwenye mchakato wako.
Na wakati sahihi utakapofika matokeo yatajidhihirisha.
Hili halimaanishi upalilie na kuficha uzembe unaopelekea ushindwe kupata matokeo unayotaka.
Unapojiambia muda ndiyo umebaki, hakikisha unafanya kwa viwango vya juu kabisa yale yote unayopaswa kuyafanya.
Hatua ya kuchukua;
Uelewe kwa kina mchakato wako wa mafanikio na ukae kwenye mchakato huo kwa msimamo. Hakikisha kila unachopaswa kufanya unakifanya ili mafanikio yako yabaki kuwa swala la muda tu.
Tafakari;
Kwenye safari ya mafanikio, hakuna njia ndefu kama njia ya mkato. Ni njia inayokupoteza na kujikuta ukihitajika kuanza tena kila wakati.
Wewe kuwa na mchakato sahihi na kaa kwenye mchakato huo huku ukijipa muda wa kutosha.
Muda ndiyo tiba sahihi ya jambo lolote lile.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed