#SheriaYaLeo (300/366); Kataa maelezo rahisi.
Sisi binadamu huwa tuna ukomo fulani kwenye uwezo wetu wa kufikiri ambao ndiyo chanzo cha matatizo mengi tunayokutana nayo.
Tunapofikiria kuhusu watu au kitu ambacho kimetokea, huwa tunakimbilia kwenye maelezo rahisi kwetu kuelewa.
Huwa tunakimbilia kwenye kuangalia kama mtu au kitu ni kizuri au kibaya, sahihi au siyo sahihi, chanya au hasi, yenye manufaa au isiyo na manufaa, yenye furaha au huzuni.
Ukweli ni kwamba kwenye maisha hakuna kitu rahisi, hakuna nyeupe na nyeusi. Watu au vitu vina mchanganyiko wa sifa mbalimbali kwa pamoja. Kunakuwa na uzuri na ubaya, usahihi na kusikokuwa sahihi, chanya blna hasi na furaha na huzuni.
Hakuna mtu au kitu chochote kwenye maisha kinachoweza kuwa na upande mmoja pekee.
Kuweza kujua pande zote za kitu kunahitaji kazi zaidi.
Watu hawapendi hilo ndiyo maana wamekuwa wanakimbilia kwenye maelezo rahisi, kitu ambacho kinawaletea matatizo zaidi.
Usiwe mtu wa kukimbilia maelezo rahisi kwenye jambo lolote lile. Badala yake zama ndani kujua pande zake zote. Itakusaidia kufanya maamuzi sahihi yatakayokuzuia usifanye makosa ya kizembe.
Sheria ya leo; Itakuwa na manufaa makubwa kwako kuongeza juhudi kwenye kuwaelewa watu au vitu kwa ndani badala ya kukimbilia maelezo rahisi ya nje. Jua vitu siyo rahisi kwa ndani kama vinavyoonekana kwa nje.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji