#SheriaYaLeo (354/366); Jichukulie umezaliwa upya.
Pale unapopitia magumu sana kwenye maisha yako na kuona kama yamefika tamati, ila ukaweza kuyavuka, unapaswa kutumia hali hiyo kuishi kwa tija zaidi.
Jichukulie kama mtu uliyezaliwa upya, ambaye umepata nafasi nyingine ya maisha baada ya kushindwa kutumia vizuri nafasi ya awali.
Kwa kujichukulia umezaliwa upya, utajali muda wako na kuishi maisha yenye kusudi.
Hutakuwa tayari kupoteza tena muda, maana unakuwa umejua thamani yake.
Hata kama hujawahi kupitia hali ya kuona maisha yamefika tamati, bado unaweza kutumia dhana hii kwa manufaa.
Kila siku mpya unayoianza, jichukulie umezaliwa upya.
Haijalishi ulifanya nini siku zilizopita, kwenye siku mpya uliyoiona una fursa ya kuanza upya.
Usiangalie umefanya au hujafanya nini siku za nyuma, unayo siku mpya ya leo, una nafasi ya kwenda kuanza upya.
Jichukulie umezaliwa upya kwenye kila siku mpya unayoianza na itumie kufanya yale ambayo ni muhimu.
Sheria ya leo; Kila siku mpya unayoipata, ichukulie kama zawadi, jione umezaliwa upya na itumie vyema kufanya yale yenye tija.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji