2896; Kupata viroboto.

Kwako rafiki yangu mpendwa unayeshangaa kwa nini mambo yako huwa yanakwama licha ya juhudi kubwa unazoweka.

Ipo kauli inayosema; ukilala na mbwa utaamka na viroboto.
Hii inamaanisha kwamba watu unaojihusisha nao huwa wanakuambukiza yale waliyonayo.

Hivyo kama utajihusisha na watu walio hasi na ambao wamekata tamaa, wanaoahirisha mambo na wasio na msukumo, hivyo ndivyo na wewe utakavyoishia kuwa.

Unapaswa kujihusisha na wale tu ambao wanakuambukiza mambo chanya na yanayokusukuma kuwa bora zaidi.

Kwenye maisha kuna washindi na washindwa.
Ukijihusisha na washindi na wewe utakuwa mshindi.
Ukijihusisha na washindwa na wewe utashindwa.

Huu siyo ubaguzi, bali ni uhalisia wa maisha.
Usimpe kila mtu nafasi, wakague kwanza watu kabla hujawapa nafasi ili wasije kukuambukiza mabaya waliyonayo.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe