3240; Ukuaji na changamoto.
Rafiki yangu mpendwa,
Changamoto na ukuaji ni vitu vinavyokwenda pamoja kwenye maisha, kila kimoja kikisababisha kingine.
Ukuaji umekuwa unaleta changamoto mbalimbali kwenye safari ambayo mtu yupo.
Na utatuzi wa changamoto ambazo mtu anakutana nazo, unapelekea ukuaji.
Ukuaji na changamoto vitakwenda pamoja kwa kipindi chote cha maisha yako.
Hivyo unapaswa kujifunza vyema jinsi ya kutumia vyote viwili kwa manufaa.
Kadiri unavyokazana kukua, jua kwamba utazalisha changamoto nyingi mpya.
Siyo hivyo tu, bali hata changamoto za zamani ambazo ulishazitatua, zinarudi kuwa changamoto kubwa zaidi.
Utatuzi wa changamoto mbalimbali unazokutana nazo unaleta ukuaji mkubwa kwenye kile ambacho mtu unafanya.
Changamoto mbalimbali tunazokutana nazo kwenye maisha ni kama mtihani wa kuvuka hatua moja kwenda hatua nyingine.
Hivyo unapotatua changamoto inayokukabili, unakuwa umeenda ngazi ya juu zaidi.
Lakini pia unakuwa umekaribishwa kwenye changamoto nyingine mpya na kubwa zaidi.
Hizi ni habari njema sana kwa wale waliochagua kucheza mchezo wa muda mrefu. Hawa ni waliochagua kile wanachofanya kuwa sehemu ya maisha yao. Hawa wanapokea kila kinachokuja na kukifanyia kazi kama inavyohitajika.
Kwa wale ambao wanatafuta njia rahisi na ya mkato ya kupata mafanikio, hizi siyo taarifa nzuri kwao.
Kwa kila changamoto wanazokutana nazo, wanaona kama ndiyo mwisho wa safari yao.
Hilo linawavuruga sana hasa kwa vile linakuwa linajirudia rudia mara kwa mara.
Pokea ukuaji na changamoto kama sehemu ya safari yako ya mafanikio.
Ukijua vyote vinaenda kwa mzunguko na hakuna kinachodumu milele.
Ukuaji utazalisha changamoto na utatuzi wa changamoto hizo utaleta ukuaji zaidi.
Hivyo ndivyo mambo yatakavyokuwa yanajirudia kwa maisha yako yote.
Utayari wako wa kuyakabili haya bila ya kuyumba ndiyo utaamua ni mafanikio kiasi gani utakayoyapata.
Hupaswi kuwa mtu wa kuyakimbia hayo, bali kuyakabili na kuyatatua mara zote.
Hivyo ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa, hatua kwa hatua.
Ukuaji na changamoto ni vitu ambavyo havina ukomo. Kadiri utakavyovikubali haraka, ndivyo utakavyoweza kunufaika navyo zaidi.
Ukuaji unazalisha changamoto.
Utatuzi wa changamoto hizo unaleta ukuaji zaidi.
Ukuaji huo wa zaidi unazalisha changamoto nyingine kubwa zaidi.
Na huo ndiyo mchezo utakaoucheza kwa maisha yako yote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante Kocha,
Nimejifunza ukuaji na changamoto vitakuwepo kwa maisha yangu yote. Wajibu wangu ni kuvikubali haraka ili niweze kunufaika navyo zaidi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ukuaji utazalisha changamoto na utatuzi wa xhamoto hizo utasababisha ukuaji zaid
LikeLike
Ndiyo mzunguko wa maisha huo.
LikeLike
Ukuaji utazalisha changamoto na utatuzi wa changamoto hizo utaleta ukuaji zaidi.
Asante sana
LikeLike
Huo ndiyo mzunguko wa maisha.
LikeLike
Ukuaji unakuja na changamoto na kutatua changamoto kunapelekea ukuaji zaidi.
LikeLike
Ndivyo mambo yanavyoenda.
LikeLike
Ukuaji unazalisha changamoto, utatuzi wa changamoto unaleta ukuaji zaidi, ukuaji huo wa zaidi unazalisha changamoto nyingine kubwa zaidi na ndio mchezo wa kucheza kwa maisha yote.
Asante sana kocha, nimekuelewa.
LikeLike
Twende na mzunguko huo, usitukwamishe pale tunapoona mambo yanajirudia na hayaishi.
LikeLike
Ukuaji unazalisha changamoto.
Utatuzi wa changamoto hizo unaleta ukuaji zaidi.
Ukuaji huo wa zaidi unazalisha changamoto nyingine kubwa zaidi.
Na huo ndiyo mchezo utakaoucheza kwa maisha yako yote.
LikeLike
Huo mzunguko haukwepeki.
LikeLike
Changamoto ni sehemu ya ukuaji wangu.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ukuaji unazalisha changamoto.
Utatuzi wa changamoto hizo unapelekea ukuaji zaidi, muhimu naona ni utayari.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Niko tayari kwa changamoto zote zitakazojitokeza na kuzitumia kama fursa ya ukuaji
LikeLike
Safi.
LikeLike