3252; Kabla ya kujifunza kushinda.
Rafiki yangu mpendwa,
Kila mtu anataka kupata ushindi mkubwa kwenye maisha yake.
Lakini wanaopata ushindi huo mkubwa na unaodumu huwa ni wachache.
Wengi huwa wanapata ushindi ambao huwa unawapoteza kabisa.
Ukweli ni kwamba kabla mtu hajajifunza kushinda, lazima kwanza ashindwe.
Ni kupitia kushindwa ndiyo mtu anajifunza mambo mengi ya kuzingatia ili kupata ushindi mkubwa zaidi na wa kudumu.
Ushindi ambao wengi wanaanza nao kwenye kile wanachofanya huwa siyo ushindi unaodumu.
Hiyo ni kwa sababu huwa hawajifunzi vizuri kwenye ushindi kama wanavyojifunza kwenye kushindwa.
Mtu anayeanza na ushindi anaweza kujisahau na kudhani yeye ana uwezo mkubwa kuliko wengine. Hilo linampa kiburi cha kutaka mambo yaende vile anavyotaka, hata kama sivyo kanuni za asili zilivyo.
Mtu anayekutana na kushindwa huwa anapitia hali ya kujifunza ambayo inamfanya aelewe vizuri kanuni za asili zilivyo.
Ni kupitia kanuni hizo ndiyo anaweza kupata ushindi mkubwa wakati mwingine.
Mtu anayeshindwa kujifunza masomo yaliyo nyuma ya kushindwa kwake ataendelea kushindwa kila mara.
Lakini anayejifunza kupitia kila kushindwa, anaendelea kuwa bora zaidi.
Katika kuitathmini biashara yoyote ile kwa haraka, angalia makosa ambayo biashara hiyo imeshapitia.
Kama kuna makosa yamefanyika lakini biashara inaendelea, maana yake kuna funzo kubwa lilipatikana kwenye makosa hayo na kuchangia kwenye ushindi.
Lakini kama unaitathmini biashara na huoni makosa ambayo biashara imeshapitia, kuwa na wasiwasi. Mafanikio yoyote unayokuwa unayaona kwenye biashara ambayo hayatokani na kushindwa, huwa ni hewa.
Kuna namna watu huwa wanavimba kichwa na kusababisha matatizo pale wanapokuwa wanapata ushindi mfululizo.
Unaposhindwa kwenye jambo lolote lile usichukie wala kukata tamaa.
Bali furahia, kwa sababu unapita kwenye darasa la kukuwezesha kupata ushindi mkubwa zaidi.
Kushindwa ni mwalimu mzuri wa kupata ushindi mkubwa zaidi, mtumie vyema.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kweli ushindi mkubwa na wa uhakika unakuja baada ya mtu kushindwa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kushindwa ni mwalimu mzuri. Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Unaposhindwa kwenye jambo lolote lile usichukie wala kukata tamaa.
Bali furahia, kwa sababu unapita kwenye darasa la kukuwezesha kupata ushindi mkubwa zaidi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha,
Kushindwa ni mwalimu wangu mkuu ili kupata ushindi mkubwa na wa kudumu.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Wale walioshindwa na kujifunza uwa wapata ushindi mkubwa
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kushindwa ni darasa zuri ili usiwe na kiburi unapopata ushindi mfululizo.
🙏🙏
LikeLike
Kweli
LikeLike
Kuna kushindwa kwingi kabla ya kushinda. Kushindwa ni kujifunza kushinda.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nikishindwa sijashindwa ila ni nimepata darasa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
kabla ya ushindi, kushindwa ni kwingi sana,na kama hujifunzi kupitia kushindwa kukata tamaa ni rahisi sana.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kushindwa hupatia mafunzo na kutufanya bora.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Tunajifunza vizuri zaidi pale tunapoanguka, hapo tunakuwa na utulivu, usikivu na unyenyekevu. Lakini Kwenye ushindi huwa kuna kujisahau, kuna kuwa na hali fulani ya kiburi na majivuno.
Asante kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni kweli kabisa. bila kushindwa katika jambo lolote huja komaa
LikeLike
Unakuwa laini mpaka ukutane na ugumu.
LikeLike
Kushindwa ni mwalimu mzuri wa kupata mafanikio tunayotaka. Kwahiyo sitakata tamaa nikishindwa
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike