3319; Kutamani na kudhamiria.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Watu wengi wamekuwa hawapati kile hasa wanachotaka, siyo kwa sababu hawawezi, bali kwa sababu wanakuwa wanatamani tu kupata.
Wanakuwa hawajadhamiria kweli kupata kitu hicho wanachojiambia wanataka.
Kwa kifupi ni kwamba watu wanakuwa wanataka matokeo makubwa, lakini hawapo tayari kulipa gharama ili kupata matokeo hayo.
Gharama za kulipa kwenye mafanikio ni nyingi, lakini kubwa zaidi ni ile nia na dhamira ya mtu kupata kila anachotaka.
Unapodhamiria kupata kitu fulani, maana yake umeachana na vingine vyote.
Hivyo vingine unavyoachana navyo vinakuwa vinaonekana vikiwa na manufaa.

Kwa sababu ya manufaa yanayoweza kuonekana kwenye kila kitu, watu ndiyo huwa wanaingia tamaa na kuona labda hiyo ni njia rahisi ya kupata wanachotaka.
Kwa kuwa kila kitu kina changamoto zake, wanapokutana na hizo changamoto wanakimbilia kwenye vitu vingine rahisi zaidi.
Hivyo ndivyo unavyokuja kukutana na mtu ambaye amefanya mambo mengi, lakini hajaweza kupata mafanikio makubwa kwenye jambo lolote lile.
Hutaweza kupata unachotaka kwa kutamani tu.
Lazima udhamirie kweli kupata hicho unachotaka.
Kwa kudhamiria kweli unaachana na vingine na kuweka juhudi kubwa kwenye hicho ulichodhamiris kukipata.
KISIMA CHA MAARIFA ni jamii ya watu ambao wamedhamiria kweli kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yao.
Ni watu ambao wameamua watafanikiwa kwenye kile walichochagua kufanya bila kujali nini wanakabiliana nacho.
Kuwa kwenye jamii hii unaachana na mambo ya kidunia ya kujilinganisha na wengine na kushindana nao hata kwa mambo yasiyokuwa na tija.
Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, unapambana na wewe mwenyewe na unajipima kwa hatua unazopiga ukilinganisha na kule unakotaka kufika.
Kwa chochote unachotaka, dhamiria kweli kukipata na siyo tu kutamani.
Weka umakini wako wote kwenye kupata hicho unachotaka.
Kwa njia hiyo utaweza kupata kile unachotaka kwa uhakika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe