
Siku moja niliingia katika duka la vifaa vya michezo, nilipofika katika duka lile nikakuta muuzaji anaongea na simu. Nikaangalia angalia nilichokuwa ninahitaji, japo sikukiona. Yule, muuzaji bado akaendelea kuongea na simu. Bila kuongea chochote. Baadaye akakata. Licha ya kukata simu, bado hakunikaribisha wala kuuliza juu ya ninachotaka. Niliangalia, kwa kuwa sikupewa usaidizi sikuona nilichokuwa nahitaji. Nikaondoka.
Je, ungekuwa ni msimamizi au meneja ungefanya nini kwa muuzaji wako? Ni suala la kutafakari.
Hali za namna hii tunaziona sana katika biashara nyingi. Unaingia eneo la biashara muuzaji anasubiri wewe uongee au uanzishe mazungumzo. Hii sio sawa. Kazi yako muuzaji ni kumkaribisha mteja na kumuongoza.
Na inapotokea, wauzaji wanakutana na mteja ambaye bado hajajua exactly huduma au bidhaa anayohitaji hawajisumbui kushughulika naye. Wanaruhusu mteja anaondoka.
Katika hali hii baadhi ya wauzaji wamejikuta wanawakosa wateja wengi kisa hawajua nini cha kuwambia, ili wawauzie.
Hali ya namna hii ikiendelea, biashara inakosa wateja na mauzo kudorola ikiwa hatoweka nguvu kujifunza zaidi juu ya nini unaenda kumwambia mteja. Je, katika hali ya kawaida, wakati wa kumhudumia mteja, ninapaswa kumwambia nini? Jibu ni rahisi, zingatia yafuatayo;
Moja; Mwambie, nina furaha kunitembelea katika biashara yangu
Mbili; Mwambie ofa iliyopo katika Biadhaa fulani
Tatu; Mwambie maslahi anayoenda kupata kutokana na huduma yako
Nne; Mwambie delivery atakayopata baada ya kukamilisha malipo
Tano; Mwambie ni kwa jinsi gani ataitaji juhudi kidogo, atapata hadhi , mauzo makubwa na mengine mengi.
Ngoja nikukumbushe kitu, wateja wamechoka kuchukua bidhaa feki, hawafiwi wala kupongezwa, hawapewi nafasi ya kuelezea maumivu yao na mengine mengi. Sehemu ya kupata faraja au huduma nzuri ni katika biashara yako. Mtue mzigo huo, usiongeze uzito.
Kuna vitu vingi unavijua ambavyo mteja akivifanya huduma yako itamsaidia kuondokana na changamoto fulani. Hilo ni jambo la kumwambia. Usiache mteja akaondoka katika biashara yako, kisa hajui anachohitaji. Haiwezekani aache biashara zingine zote aje kwako.
Hatua za kuchukua leo: Mteja yeyote anakuja katika biashara yako, iwe kwa bahati au kwa kupenda usiache akaondoka bila kuongea naye. Chukua hata namba ya simu Kwa matumizi ya baadaye.
Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo na Mwandishi. Tuwasiliane 0767702659. Karibu tujifunze zaidi.