Ofa ni faida au thamani ya ziada inayotolewa kwa mteja ili kumshawishi kununua. Kisaikolojia sisi binadamu tunapoona neno ofa au kupewa ofa tunafanya maamuzi haraka ya kununua.

Naamini hata wewe kuna bidhaa ulishawishika kuzinunua Kwa sababu ya ofa walizoweka wauzaji.


Taasisi ya Neuromarketing Researchers walifanya utafiti kuhusu  “psychological of discount” na kugundua kwamba;

Asilimia 70% ya wateja hutafuta bidhaa zenye ofa kwanza kabla ya kununua.

Asilimia 66% ya “couple” yaani wawili wapendanao hufanya maamuzi ya kununua bidhaa zenye ofa hata kama hawakuwa na mpango wa kununua

Asilimia 80% ya mtu mmoja mmoja hununua bidhaa zenye ofa.

Kwahiyo unaweza kuona ni kwa namna gani katika ufuatiliaji wa wateja wako ukitumia ofa kwenye baadhi ya ofa ni rahisi kuwashawishi kununua.

Aina za ofa;

Moja; Ofa ya punguzo la bei
Hapa unapunguza bei ya bidhaa kutoka kwenye bei ya awali. Mfano, simu inauzwa 275,000/= mteja unampatia punguzo la sh..5000/=au 10000/=

Mbili; Ofa ya nyongeza ya bidhaa
Hii ni aina ya ofa unayoongeza bidhaa. Mfano, unapokunua kumpyuta unapata external GB 2.5, Mouse na Begi bure.

Tatu; Ofa ya kupelekewa bidhaa(free delivery).
Mfano, mteja ananunua mlango, Tv, kitabu au bidhaa nyingine, wewe unaingia unafikisha bidhaa alipo mteja.

Nne; Ofa ya mafunzo au ushauri bure.
Hapa unamwambia mteja kwamba, ukinunua kitabu cha “MAUZO NI MCHEZO WA NAMBA” utapata ofa kupewa ushauri bure kuhusu kujua namba za biashara yako.


Tano; Ofa ya usimamizi
Mfano, mteja ananunua kitabu cha unamsimamia kusoma bure. Ananunua vifaa vya umeme au bomba unampatia usimamizi wakati wa ufungaji wa vifaa hivyo bure.

Manufaa unayopata kwa kutoa ofa kwa wateja wako ni;

Moja; Kutofautisha biashara yako na nyingine.
Sio kila biashara inatoa ofa, hii ni kwa sababu tofauti za kimahitaji, soko, kimkakati na zingine.

Mbili; Kumvuta mteja katika biashara yako
Hii ni kwa sababu punguzo la pesa analopata mteja linamsaidia kufanya mambo yake mengine.

Tatu; Kumchochea mteja kufanya maamuzi.
Kinachofanya wateja kufanya maamuzi kwa sababu ofa ina ukomo, haiwi siku zote.

Nne; Kukusaidia kuuza bidhaa ambazo haziuziki.
Mfano wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani au sikukuu zingine Kuna ofa zinatolewa. Hii inasaidia kuuza zaidi hata zingine zilizokiwa zimekaa ndani kwa muda mrefu.

Hatua za kuchukua leo, andaa bidhaa moja, iweke kwenye ofa itangaze. Wakati wa mauzo mpendekezee bidhaa zingine ili ikusaidie kuziuza pia.

SOMA; Mauzo Ya Ziada Na Namma Yanavyokuza Biashara Yako


Je, ni ofa ipi umewahi kuwapa wateja wakanunua zaidi? Shirikisha hapa tujifunze kutoka kwako.

Wako Wa Daima
Lackius Robert

Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi

0767702659 | mkufunzi@mauzo.tz