3419; Ng’ombe anayetoa maziwa.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Unapokuwa na ng’ombe anayetoa maziwa, unafanya naye nini?
Jibu ni moja, unamkamua maziwa hayo.
Utaendelea kumkamua maziwa kwa kadiri yanavyokuwa yanatoka.
Hutachoshwa na ng’ombe huyo na kutaka kumbadili, anatoa maziwa na unamkamua.

Cha kushangaza, inapokuja kwenye fursa mbalimbali, ambazo zina manufaa kwako, umekuwa huwezi kukaa nazo kwa muda mrefu.
Hata pale ambapo fursa bado ina manufaa, huwa huwezi kuendelea nayo kwa muda mrefu.

Sababu ya kufanya hivyo ni kuchoshwa na kurudia rudia kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu bila kuacha.
Unapata msukumo wa kujaribu vitu vya tofauti na hapo ndiyo unaharibu kitu ambacho kinafanya kazi na kwenda kuangukia kwenye kitu ambacho hakifanyi kazi.

Rafiki, unapopata ng’ombe anayetoa maziwa, wajibu wako namba moja ni kumkamua mpaka tone la mwisho.
Usiache ndani yake hata kidogo, toa kila kinachoweza kutoa.

Unachopaswa kufanya ni kuendelea kuangalia fursa nyingine kwenye hicho ambacho tayari unakifanya na kinakupa matokeo mazuri, kabla ya kuhangaika na mambo mapya.

Kama kitu kinafanya kazi vizuri, endelea kukifanyia kazi kwa manufaa kabla ya kukibadili.
Usichoshwe na hitaji la kurudia rudia kufanya kila mara.
Pendelea matokeo ya uhakika yanayopatikana kwenye kitu.
Na ongozwa na nayo mara zote.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe