Rafiki yangu mpendwa,

Kuna njia nyingi za kujenga utajiri, lakini siyo zote ni sahihi.

Kuna watu ambao huwa wanapata utajiri kwa njia ambazo hata wao wenyewe hawawezi kuzirudia kwa uhakika.

Chukua mfano wa mtu aliyepata utajiri kwa kushinda bahati nasibu, ni vigumu kwake kurudia tena kushinda.

Kadhalika kuna njia ambazo baadhi ya watu wanaweza kuzitumia, ila wengine hawawezi kuziiga. Mfano wa mtu anayepata utajiri kwa kurithi, kama huna mtu wa karibu mwenye mali unazoweza kurithi, huwezi kutumia njia hiyo.

Lakini zipo njia za kujenga utajiri ambazo zipo wazi kwa watu wote. Njia hizo zinaweza kutumiwa na mtu yeyote bila ya kikwazo chochote kile kwenye kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yao.

Mwandishi na bilionea Ken Fisher, kwenye kitabu chake kinachoitwa THE TEN ROADS TO RICHES ameshirikisha njia 10 za kujenga utajiri zinazoweza kutumiwa na mtu yeyote ambaye amedhamiria kwenye hilo.

Tumekuwa na mfululizo wa masomo ya njia hizo 10 za kujenga utajiri pamoja na hatua unazoweza kuchukua kwenye kila njia. Masomo yote yanapatikana kwa KUBONYEZA MAANDISHI HAYA.

Tumekuwa na mjadala wa njia hizo 10 za kujenga utajiri, ambapo washiriki wameweza kueleza njia ambazo wapo na njia ambazo wangependa kufikia katika kujenga utajiri. Pia wameshirikisha hatua wanazochukua kwenye USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI.

Karibu usikilize mjadala huo na pia uweze kushirikisha yale uliyojifunza kwa kuweka maono hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.