Ukikimbizwa na mbwa mkali, unaweza kupanda ukuta mkubwa.
Ukiambiwa urudie kupanda ukuta huo bila ya uwepo wa mbwa anayekufukuza, unashindwa.

Hivyo ndivyo mafanikio yalivyo, siyo tu kufanya jambo gumu mara moja ndiyo kutakupa mafanikio.
Bali kufanya kwa kurudia rudia kwa muda mrefu bila kuacha.

Jijengee uwezo wa kufanya mambo magumu kwa mwendelezo na utaweza kupata mafanikio makubwa kadiri ya unavyotaka.

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE | +255678977007 | https://bit.ly/makirita