3538; Mauzo ya kimafanikio.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Maisha ni mchezo mkubwa sana wa mauzo ambapo kila mtu ni muuzaji.
Na mafanikio ambayo watu wanapata yanategemea sana nini wanauza na kwa ukubwa kiasi gani.
Matajiri wanauza suluhisho la matatizo au mahitaji ambayo watu wanayo.
Popote penye watu kwao ni fursa.
Wanachoangalia ni watu hao wana matatizo au mahitaji gani, kisha wanawauzia suluhisho.
Kwa sababu watu huwa hawapo tayari kuendelea kuumia na matatizo wanayokuwa nayo, wanakuwa tayari kutoa fedha kuyatatua.
Na hapo ndipo matajiri wanapozidi kutajirika.
Masikini wanauza matatizo waliyonayo kwa wengine. Wanapokutana na wengine wanafanya kazi kubwa ya kueleza matatizo yao na jinsi yanavyowakwamisha.
Masikini wanaenda mbali zaidi na kushindana na wengine nani mwenye matatizo zaidi.
Kwa sababu masikini wanauza matatizo, kwa masikini wenzao ambao nao wana matatizo, hakuna pesa wanapata.
Hata wakisaidiwa, ni kidogo tu na imekuwa haiwatoshelezi.
Watu wenye ndoto kubwa wanauza maono. Wanakuwa na picha ya kule wanataka kufika na kuwaonyesha wengine jinsi ambavyo watanufaika kwa kufika huko.
Kwa kuwa wanakuwa wanayaamini sana maono waliyonayo, huwa wanakuwa na ushawishi mkubwa na unaowavutia watu wengi kwao.
Kwa kuwa na wengi, wanafanya makubwa.
Watu wavivu na wazembe huwa wanauza visingizio. Hawa huwa na sababu na visingizio kwa nini vitu haviwezekani.
Waonyeshe fursa nzuri kwao kupiga hatua na watakuambia haiwezekani.
Waonyeshe wengine ambao imewezekana kwao na watakuambia wao ni tofauti.
Rafiki, wewe unauza nini?
Usijiambie kujifariji, bali jiambie kulingana na matokeo uliyonayo sasa.
Kisha chukua hatua ya kuuza kilicho sahihi kulingana na matokeo unayotaka kupata.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe