Wengi wetu tunajua mazoezi yana faida kubwa sana mwilini. Baadhi ya faida hizo ni kuimarisha afya, kuongeza ukakamavu, kupunguza mawazo na kupunguza unene kama wengi wanavyofanya. Lakini wengi wetu tunaposikia neno mazoezi moja kwa moja tunafikiria mazoezi ya mwili, yaani kukimbia, kubeba vitu vizito na michezo mbalimbali.
Kuna zoezi la msingi sana ambalo wengi wetu hatulifanyi japo ndilo zoezi muhimu maishani, zoezi hilo ni zoezi la akili. Kama ilivyo kwa mazoezi mengine ya mwili, zoezi la akili ni muhimu kwani linaimarisha uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo. Linakufanya uweze kutumia akili yako kutatua tatizo lolote utakalokumbana nalo. Pia zoezi hili litakufanya uweze kupata njia bora za kufikia malengo yako maishani.
Unajiuliza unaweza vipi kufanya zoezi la akili? Ama zoezi la akili ni lipi? Zoezi la akili ni kufikiria na ninaposema kufikiria namaanisha kufikiria kuliko na tija na sio kufikiria juu ya hofu. Fikiria juu ya malengo yako ama fikiria njia za kutatua matatizo uliyo nayo. Na kufikiria huko hufikirii tu popote ulipo ila unakuwa na utaratibu maalumu wa kufikiria.
Kila siku tenga angalau nusu saa na ukae sehemu ambayo hakuna kelele wala muingiliano wowote, inaweza kuwa kwenye chumba ama sehemu yoyote ambayo utakuwa na utulivu, hata simu izime. Kuwa na kalamu na karatasi ama kijitabu ambacho utakuwa unakitumia kwa kazi hiyo tu, kuandika mawazo. Andika lengo unalotaka kufikia ama tatizo unalotaka kutatua kwenye kijitabu chako na ufikirie njia za kuweza kufikia ama kutatua. hakikisha kwa muda huo hufikirii kingine chochote zaidi ya ulichopanga, na fikiria mpaka utakapopata majibu zaidi ya kumi.
Kwa kusoma hivi unaweza kuona ni kitu rahisi sana kufanya ila kwa mwanzo ni ngumu mno hivyo inabidi utengeneze nidhamu ya kuweza kufanya hivyo. Akili ya binadamu kwa dakika moja inaweza kuwaza mambo zaidi ya mia moja yasiyo ya msingi. kwa mfano kama umeingia kwenye chumba kwa ajili ya kufikiri unaweza kujikuta unafikiri vitu ambavyo havina uhusiano kabisa kwa mfano nitapigiwa simu, watu watanionaje kwa kila siku kukaa peke yangu kwa muda fulani, nitavaa nguo gani, magazeti ya leo yameandika nini, kuna jipya gani facebook na mengine mengi. Mawazo hayo yanapoteza zaidi ya asilimia 80 ya muda wako wa kufikiri. Lazima ujifunze kuondokana na mawazo haya na kufikiria lile ulilokusudia kulitatua.
Japo mwanzo itakuwa ngumu ila ukiweza kufanya hivyo kwa wiki tatu basi itakuwa ni tabia na hutaona tena shida, na utaweza kuongeza kutoka nusu saa mpaka saa moja ya kufikiria kwa siku. Kama unaweza kupata mawazo kumi kwa siku, hamsini kwa mwezi na mia tatu kwa mwaka basi kufikia malengo yako itakuwa rahisi sana kuliko unavyodhani kwa sasa.