Mwaka 2013 umekwisha na sasa ndio tumeingia kwenye mwaka mpya kabisa 2014. Kuna mambo mengi ulipanga kufanya mwaka 2013, kuna ambayo ulifanikiwa kufanya na kuna ambayo ulishindwa kuyatimiza. Pamoja na yote hayo mwaka ndio umeshakwisha na sasa tupo kwenye mwaka mwingine.

               2014

  Blog yako AMKA MTANZANIA imekuwa nawe kila siku kwa mwaka 2013. Umekuwa ukijifunza na kuhamasika kupitia makala mbalimbali ulizosoma kwenye blog hii.

  Nipende kuchukua nafasi hii kukutakia heri ya mwaka mpya 2014. Najua umeshaweka malengo na mipango mikubwa kwenye mwaka huu.

  Naahidi kuwa nawe kwenye safari yako ya kutimiza malengo yako ya mwaka 2014 na miaka mingi ijayo. AMKA MTANZANIA itakuwepo kila siku kukutia moyo, kukuelimisha na kukuhamasisha pale unapopitia vikwazo mbalimbali.

  Mwaka 2014 utakuwa na mambo mengi mazuri hapa AMKA MTANZANIA ambapo hakuna msomaji atakayeachwa nyuma. Mwaka 2014 utakuwa mwaka wa mageuzi kwa wasomaji walioamua kuchukua hatua juu ya maisha yao.

  Baadhi ya mambo makubwa yatakayofanyika mwaka 2014 ni;

1. Kutoa kitabu ambacho kitakuwa nguzo kubwa ya mabadiliko kwenye maisha ya wasomaji.

2. Kutoa semina nne kwa wakazi wa dar es salaam na maeneo ya karibu.

3. Kutoa semina kwa njia ya mtandao kwa watakaoshindwa kuhudhuria semina.

4. Ushauri wa ana kwa ana kwa wale waliochoshwa na maisha wanayoishi na wameamua kubadilika na kwa wenye miradi mbalimbali wanayotaka kufanya.

  Kwa hayo na mengine mengi yataufanya mwaka 2014 kuwa mwaka wa kihistoria kwa msomaji atakaechukua hatua ya ziada.

  Semina ya kwanza itafanyika dar es salaam jumamosi ya tarehe 18/01/2014 kama bado hujajiandikisha kushiriki bonyeza maandishi haya kisha ujaze fomu ya ushiriki.

  Nikushukuru sana wewe msomaji kwa kuwa sehemu ya mafanikio makubwa ya AMKA MTANZANIA. Pia nikutakie kila la kheri kwenye mwaka huu mpya 2014.

  Tutaendelea kuwa pamoja na kwa wale watakaofanya maamuzi thabiti ya kubadili maisha yao wataona mabadiliko makubwa sana kwa mwaka 2014 na kuendelea.

  Tafadhali sema heri ya mwaka mpya kwenye maoni hapo chini kama tuko pamoja.