Mbinu 5 Za Kukuwezesha Kuishi Maisha Ya Malengo.

Siri kubwa ya kufikia mafanikio unayoyahitaji katika maisha yako ni kuhakikisha unaishi maisha yanayoendana na malengo yako. Kinyume na hapo utakuwa ni mtu wa kupoteza muda wako kutokana kuishi maisha yasiyo na mwelekeo kitu ambacho ni hatari kwako.
Ili uweze kufanikiwa hiki ni kitu ambacho hutakiwi kukwepa hata kidogo. Jukumu kubwa unalotakiwa kulitambua ni kuelewa misingi na malengo yako unayotakiwa kuyafuata kila siku bila kupotea. Je, ni mbinu zipi unazoweza kuzitumia ili zikusaidie kuishi maisha yenye malengo?
1. Jifunze kusema HAPANA.
Watu wengi kutokana na kuwaogopa au kuwahofia watu waliokaribu nao, hujikuta wao ni watu wa kukubali karibu kila kitu wanachoambiwa  hata kama kitu hicho kinawabana. Hiki ni kitu ambacho kinaonekana kuwa kigumu kwa wengi hasa linapokuja suala la kusema HAPANA.
Kwa bahati mbaya sana kutokana na hilo wengi hujikuta wakiishi maisha ya kuyumbishwa yasiyo na msimamo wala malengo. Ili uweze kuishi maisha ya malengo na kuishi maisha yako ni lazima kujifunza kusema HAPANA kwa mambo mengi usiyaelewa kwako. Hilo litakusaidia sana kuishi kwa malengo siku zote.
2. Kuwa makini na muda wako.
Vipo vitu vingi unavyoweza kuvipoteza katika maisha yako ukavipata lakini siyo muda. Muda ulionao ni wa thamani sana na kwa bahati mbaya ukishaupoteza umepotea kabisa hauwezi kurudi tena. Hiyo yote ni dalili tosha inayoonyesha kuwa kuna uthamani mkubwa ulio ndani ya muda wako ambao hutakiwi kuupoteza.
Sasa kama wewe unaishi maisha ya kupoteza muda sana, inabidi uelewe kuwa hivyo ndivyo unavyopoteza maisha yako na mwisho wa siku unajikuta ukiishi maisha yasiyo na malengo kabisa ikiwa na pamoja utakosa mafanikio. Unaweza usilione hili mapema sana lakini  kwa kadri unavyozidi kupoteza muda wako nafasi ya kufanikiwa inakuwa ndogo.
3. Sahau yaliyopita.
Itakuwa haina maana sana kwako kama utaendelea kungang’ania mambo mengi ambayo yameshapita. Hiyo itakuwa ni sawa na kupoteza muda. Maisha siku zote ni kusonga mbele na wala siyo kurudi nyuma. Sasa basi, inapotokea sehemu umekosea, jifunze kutokana na makosa hayo kisha endelea mbele.
Utakuwa ni mtu ambaye huishi kwa malengo ikiwa utazidi kushikilia, kujilaumu na kung’ang’ania mambo yaliyopita. Tafuta mwelekeo na dira mpya itakayokufanya uzidi kufanya mambo yako kwa upya hadi kufanikiwa zaidi na tena kwa viwango vya juu.
4. Tambua mambo yapi ni ya muhimu kwako.
Siyo kila kitu ni cha muhimu kwako. kwa maana hiyo ni muhimu kuyachagua mambo ambayo ni muhimu na ya lazima katika maisha yako na kama ni kuyatekeleza ndipo uanzie hapo. Kama ni malengo chagua yale kwanza ya muhimu kwako, kisha utekelezaji ufuate.
Acha kujidanganya kuwa kila kitu ni cha muhimu kwako. Na kama utazingatia kila kitu na kukiona ni cha muhimu kwenye maisha yako basi, utakuwa umepotea. Hii ni kwa sababu utajikuta mambo yako mengi unashindwa kuyakamilisha kutokana na kukosa uzingativu kwa kile unachokifanya.
5. Jiwekee malengo kila wakati.
Hiki ni kitu ambacho hupaswi kukisahau hasa linapokuja suala la kuweka malengo. Mara nyingi malengo unapokuwa nayo yanakuwa yanakupa mwelekeo wa kuweza kusonga mabele na kukupa hamasa zaidi. Unaweza ukajiwekea malengo ya muda mrefu au ya muda mfupi hata kwa siku ili yakupe mwelekeo sahihi na kuishi maisha ya malengo.
Kwa vyovyote vile unahitaji kuishi maisha ya malengo ili uweze kufikia mipango na malengo makubwa uliyojiwekea katika maisha yako.
Nakutakia mafanikio mema kwa kile unachokifanya na endelea kutembelea  AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza na kuboresha maisha yako.
Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika zaidi.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
 Imani Ngwangwalu,
0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: