Networked blogs ni program ya kwenye mtandao ambayo inakuwezesha kuunganisha blog yako moja kwa moja na mitandao ya kijamii ambayo ni facebook na twitter. Kwa kuwa na akaunti kwenye networked blogs utaunganisha account yako ya twitter, faceebook, page za facebook unazomiliki na magroup ya facebook unayosimamia.

Kwa kuwa na program hii kila unapopuplish post kwenye blog yako inapelekwa moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii. Pia inakuwa sehemu rahisi kwa wewe kushare post yako kwenye magroup na pages zako kwa wakati mmoja. Na pia watu wanaweza kukufuata na kusoma blog yako kwa kutumia networkedblogs.

Kuweka blog yako kwenye networked blogs fuata hatua zifuatazo;

1. Nenda www.networkedblogs.com utaona kama kwenye picha hapo chini.

nwb

2. Unaweza kulog in kwa kutumia akaunti yako ya facebook au unaweza kubonyeza ADD YOUR BLOG na ukatengeneza akaunti mpya.

3. Ukibonyeza log in kwa kutumia facebook utafuata maelekezo ya kuweka username na password yako na baadae utakubali. Baadae utapata hatua kama  inavyoonekana hapo chini

 

nwb3

4. Bonyeza Next, chagua blog utakazozifuata, kisha bonyeza tena next, endelea tena.

5. Baadae utafikia hatua nwb4kama inavyoonekana hapo chini, bonyeza ADD MY BLOG.

 

 

 

 

 

 

 

 

6. Utaenda kwenye bashboard kama inavyoonekana hapo chini, bonyeza REGISTER A BLOG au unaweza kubonyeza CREATE MY BLOG FOLLOWER

nw5

7. Baada ya hapo itakuletea sehemu ya kuweka address ya blog yako. Weka adress, kisha nenda next. Itakuletea sehemu ya kujaza na sehemu zilizowekewa alama ya nyota ni muhimu kujaza. Mfano kwenye FEED LINK weka feed ya blog yako, ukishaweka adress yako FEED yako inakuja moja kwa moja. Picha ni kama hapo chini.

nw7

nw8

8. Baada ya kujaza taarifa hizo bonyeza does not contain nudity kisha bonyeza next next.

9. Utaulizwa kama wewe ni author wa blog uliyoweka bonyeza yes.

10. Itakuja step ya get confirmed as author, bonyeza INSTALL WIDGET.

11. Copy hizo code na uende kuweka kwenye WDGET ZA PEMBENI kwenye blog yako.

Baada ya hapo bonyeza VERIFY NOW.

NW10

12. Angalia pembeni bonyeza SYNDICATION

 

nw12

13. Chagua blog yako, chagua send verification again baada ya hapo utaverify.

nw13

14. Baada ya kuverify rudi kwenye dashboard na syndicate kisha chagua account zako za mitandao ya kijamii ambapo utakuwa unashare.

nw14

Baada ya hapo tayari una akaunti yako ya networked blogs na ukitaka kushare unaingia huko na kuchagua ni makala gani unashare.

Kila utakapoweka post mpya kwenye blog yako inapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti ulizounganisha.