Dalili Za Kujua Kama Utakufa Maskini Au Tajiri.

MAKALA HII IMEANDIKWA NA IMANI NGWANGWALU WA TANGA TANZANIA.

Kila mmoja wetu kwa jinsi alivyo ana namna yake ya kufikiri na hizi namna tofauti za kufikiri ndizo ambazo zinatofautisha binadamu. Ni tofauti hizi pia ambazo zinatufanya tuwe na tofauti katika mafanikio maishani mwetu. Wale ambao wanafikiri vizuri na kuamini katika kumudu, huwa ndio wanaofanikiwa sana. Wale ambao wanafikiri vibaya na kuamini katika kushindwa, siku zote huwa wanaanguka.

Wataalamu wa masuala ya mawazo na mafanikio wanabainisha vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtu kutabiri kama maisha yake yatakuwa ni kushindwa hadi mwisho au yatakuwa ni ya mafanikio.Zifuatazo ni dalili za kujua kama utakufa maskini au tajiri:-

1.Kama unaamini mafanikio yapo kwa ajili ya watu wachache na maalum, ujue kabisa utakufa maskini. Inaelezwa kwamba kama mtu akiwa anaamini kwamba kuna watu wengine wa aina fulani, mahali fulani ambao ndiyo peke yao wanaoweza na kufikia juu kwenye kilele cha mafanikio, mtu kama huyo hawezi kamwe maishani mwake kuja kutoka kwenye lindi la umaskini.

Hawezi kutoka kwenye lindi la umaskini kwa sababu juhudi zake ambazo zingemfikisha mbali zinakuwa tayari zimewekwa mipaka na imani hiyo kwamba yeye hahusiki katika kufanikiwa, bali kuna wengine ambao wamepangiwa kufanikiwa. Kwa kufikiri hivyo juhudi yake kubwa katika kutafuta itakuwa ni ile kumfanya asife kwa njaa na siyo kutoka hapo alipo. Kama tujuavyo tunapoamini jambo fulani mawazo yetu hutusaidia kulifikia jambo hilo.

Kwa kuamini hivyo mazingira tunayoyajenga ni yale ya kutusaidia kuishi kwa kupata riziki tu.Hata kama fuko la fedha litadondoka miguuni mwetu tutalipiga teke na kuliambia mimi sikuandikiwa kupata bwana, kuna wenyewe. Hali kama hii hujitokeza mara nyingi sana maishani mwetu. Tunakabidhiwa dhamana kubwa ambayo ingetusaidia sana maishani mwetu lakini tunacheza nayo hadi inapotea kwa sababu tu hatuamini kwamba tunastahili kuitumia kufika juu. Tunaziona nafasi za kusonga mbele lakini tunaamini kwamba hatustahili kuzitumia na mwisho wake tunabaki kushangaa ni kwanini tunashindwa kuinuka katika mazingira magumu tuliyomo.

kazi inayolipa

2. Kama unaamini huwezi, umeshindwa kutokana na sababu mbalimbali, hiyo ni dalili pia ya kukuonyesha kuwa utakufa maskini.

Wataalamu wa elimu ya mafaniko wameeleza kwamba kamwe mtu huyu hawezi kuja kuvuka kizingiti cha umaskini.Kuna watu ambao kutokana na sababu mbalimbali walifanywa kuamini kwamba hakuna wanachoweza kutokana na malezi, mazingira au uzoefu mbalimbali wa kimaisha.

Mtu anapoamini kwamba hawezi anayaambia mawazo yake ya kina yamsaidie kumfanya ashindwe zaidi kwenye kila jaribio analolifanya.Baala ya kufanya juhudi kujisaidia ili amudu, hujibwetesha kwa kuamini kwake kwamba hata kama atafanya kitu gani, kamwe hata mudu. Siyo rahisi kwa mtu mwenye mawazo ya namna hii kufanikiwa maishani.

Kuna watu kwa kukosa kitu fulani ambacho jamiii inakiona kama ndiyo ufunguo wa maisha (Mafanikio), huwa wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa na kufanya vizuri kama hao ambao wanacho. Kwa mfano, kwa kukosa elimu, ujuzi au utaalamu fulani,watu wengine hujihesabu wanyonge. Huchukulia kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na utaalam fulani ndio wanaoweza au wanaotakiwa kufanikiwa.

Bila shaka umewahi kusikia au hata wewe mwenyewe kusema “Si wamesoma bwana, ndiyo wanaojaliwa, sisi ambao hatuna elimu kazi yetu itakuwa kuwatumikia” Kauli kama hizi zina chimbuko lake mbali sana, pengine katika malezi yetu. Wazazi walizoea au wamezoea kuwaambia watoto wao “usiposoma kazi yako itakuwa ni kuwabebea wenzako mizigo” Kwa bahati mbaya mtoto aliyelishwa ‘sumu’ hii anaposhindwa shule, huamini kwamba yeye kwamba atabaki kutumikia wengine tu.

Kitu usichojua unaweza kufanya mambo makubwa katikati ya udhaifu wako huna bahati mbaya hata kidogo,kama unafikiri natania kamuulize Jesca Convex huyu ni mwanadada ambaye alizaliwa hana mikono yote miwili lakini kwa sasa ni rubani anatumia miguu yake kuendeshea ndege, ulemavu wake haukumzuia kufikia ndoto zake, unajifunza nini hapo? jiulize kwa nini huwezi? Kwanini uko hapo? Unaamini udhaifu? Udhaifu si kitu.

Kumbuka tunapoamini hatuwezi kufika kwenye mafanikio kwa sababu mbalimbali hatuwezi fika mbali. Moja ya vigezo muhimu vya kutufikisha kwenye mafanikio ni kuamini kwetu kwamba tunaweza kufika huko.Tunapokuwa hatuna imani kwamba hatuwezi kufika huko tunajifungia njia wenyewe.

3. Mtu ambaye anaamini kwamba ana mikosi, balaa au nuksi na pengine laana ambazo zinamzuia kufikia malengo yake.

Wengi wetu huwa tunaamini hivyo tuna mikosi, nuksi, balaa na laana chungu nzima.Tunaamini hivyo kiasi kwamba hata tukifikia karibu kabisa na mafanikio huwa tunajiambia ni kazi bure,tutaporomoka tu na kweli kwa kuamini hivyo hujikuta tukiporomoka kila tukifikia karibu na kufanikiwa au kufikia malengo.

Kinachotekea ni kwamba,kwa kuamini kwetu kuwa tuna mikosi,balaa,laana au nuksi huwa tunatenda kwa mkabala huo wa kinuksi au kibalaa na kimkosi, ambapo matokeo yake ni kujikwamisha.

Wataalamu wa elimu ya mafanikio wanaeleza kwamba tunapoamini kuwa tuna mikosi au nuksi huwa tunayashauri mawazo yetu ya kina kutusaidia kuendelea kuwa katika hali hizo. Ndiyo maana sio rahisi kukuta mtu anayeamini katika nuksi kuondoka katika hali hiyo.

Kwa hiyo, kama unaamini kabisa kutoka moyoni mwako au unahisi kwamba wewe huwezi kamwe kufika popote ,utakufa maskini. Kikubwa zaidi hujachelewa kwa sababu umelifahamu hilo, unachotakiwa kufanya ni kubadili hiyo imani yako kwa sababu mafanikio hayachagui mtu, umri, rangi, taifa au jinsia bali mtu anavyoamini katika mafanikio na kutenda.

UNAWEZA KUWASILIANA NA MWANDISHI WA MAKALA HII IMANI NGWANGWALU KWA 0767048035.

KAMA NA WEWE UNA MAKALA NZURI ULIYOANDIKA NA UNAFIKIRI INAWEZA KUWAAMSHA WATANZANIA TAFADHALI NITUMIE KWENYE amakirita@gmail.com

MAKALA ISIWE IMEWEKWA KWENYE BLOG AU CHOMBO KINGINE CHA HABARI, IWE IMETUMIA KISHWAHILI RAHISI NA KINACHOELEWEKA NA IWE NA MANENO KATI YA 500 NA 1000 KARIBU SANA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: