Nilipoandika makala ya jinsi tabia ya kujisomea imekuwa na manufaa kwenye maisha yangu watu wengi sana wameniuliza inawezekanaje naweza kusoma vitabu vingi hivyo. Kwenye makala ile niliandika mwaka 2012 nilisoma vitabu zaidi ya 120, mwaka 2013 vitabu zaidi ya 70 na mwaka huu 2014 ninasoma angalau kitabu kimoja kila wiki(kama hukuisoma bonyeza maandishi haya kuisoma makala hiyo). Unajiuliza nawezaje kusoma vitabu vyote hivi? Au unafikiri sina kazi nyingine za kufanya zaidi ya kusoma vitabu tu? Hapana, niko bize kama ulivyo wewe, tena nikikueleza ratiba yangu ya siku huenda nikawa bize mara mbili yako.
Kama unataka kuboresha maisha yako mara kumi ya ubora ulioko nao sasa soma vitabu 30. Nakuhakikishaia kwa muda ambao utakuwa umemaliza kusoma vitabu hivyo 30 utakuwa mtu wa tofauti sana na ulivyo sasa hivi. Kwani utakuwa umebadili mtazamo wako kuhusu maisha na watu wengine, utakuwa umejijengea ujasiri, utakuwa umeondoa hofu zisizo za kweli, na utakuwa umejifunza tabia muhimu za kukuwezesha wewe kufikia mafanikio kama matumizi mazuri ya muda, uaminifu, kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa na matumizi mazuri ya fedha zako.
Vitabu 30 tu ndio unahitaji kuvisoma, na ukishavisoma……. UCHUKUE HATUA. Maana hakuna kitakachotokea kama hutachukua hatua.
Swali ni je unawezaje kusoma vitabu 30 huku tayari siku yako imejaa, yaani huna hata dakika moja ya kuwekeza kusoma?
Nakupatia suluhisho rahisi ambalo litakusaidia kujifunza hata kama huna muda.
Njia unayoweza kutumia hapa ni kuwa na AUDIO BOOKS, yaani vitabu vilivyosomwa. Kwa kuwa na vitabu hivi utaweza kuvisikiliza kwenye simu, kwenye gari, kwenye redio na kadhalika. Kwa kuwa na vitabu hivi, muda ambao unasafiri kwenye gari au uko kwenye foleni unasikiliza, ukiwa unamsubiri mtu unasikiliza, ukiwa unapumzika unasikiliza na hata wakati unajiandaa unaweza kuwa unasikiliza. Ni njia rahisi sana ya kujifunza ambayo haitavuruga ratiba yako uliyonayo sasa, na utaongeza ujuzi mkubwa sana kwako.
Unajiuliza utapata wapi AUDIO BOOKS?
Ili kukusaidia kupata vitabu vilivyosomwa nimeandaa memory card yenye vitabu 25 vilivyosomwa. Memory kadi hii unaweza kuiweka kwenye simu yako(hata kama ni ya kichina, kwenye gari au hata kwenye kompyuta au redio).
Vitabu 25 vilivyopo kwenye kadi hii ni;
1. Cashflow quadrant – R. Kiyosaki
2. Rich dad poor dad – R. Kiyosaki
3. Increase your financial IQ – R. Kiyosaki
4. Freedom or security – R. Kiyosaki
5. Retire Young Retire Rich – R. Kiyosaki
6. Brian Tracy – Become an Outstanding Manager
7. Brian Tracy – 21 Success Secrets of Self-Made Millionaires
8. Brian Tracy – Get Paid More and Promoted Faster
9. Brian Tracy – How To Gain 2 Extra Hours a Day
10. Brian Tracy – 21 Ways to Build a High Profit Business
11. Brian Tracy – 21 Ways To Get Ahead In Your Career
12. Brian Tracy – Make a Million
13. Brian Tracy – The Psychology of Achievement
14. How To Instantly Connect With Anyone
15. Napoleon Hill’s Keys To Success
16. Anthony Robbins – Awaken the Giant Within
17. Brian Tracy – 21 Great Ways To Manage Your Time And Double Your Productivity
18. Zig Ziglar – How To Be A Winner
19. Zig Ziglar – Success And The Self-Image
20. Earl Nightingale – Lead The Field
21. James Allen – As A Man Thinketh
22. Kerry L. Johnson – Science of Self Discipline
23. David Lieberman – Get Anyone To Do Anything
24. Eric Ries – The Lean Startup
25. Outside Your Comfort Zone – Jeff Lilley
Kadi hii inapatikana kwa tsh elfu kumi na tano(15,000/=) na inatolewa kwa muda mfupi tu. Hivyo kama unaitaka kadi hii unaweza kuipata kwa siku ya jumamosi tarehe 07/06/2014 na inabidi utoe taarifa za kuihitaji memory kadi hii kabla ya siku ya ijumaa kuisha. Nasema utoe taarifa mapema ili niweze kukuandalia kadi hii.
Wakati unatoa taarifa unatuma na fedha kwa MPESA 0755953887 au TIGO PESA 0717396253 kisha jumamosi utapewa kadi yako.
Kwa wale wa mikoani kadi itatumwa kwa basi siku hiyo ya jumamosi na hivyo unatakiwa kutuma fedha ya kadi na fedha ya nauli kabla ya ijumaa. Kadi ti tsh 15,000/= na nauli ni tsh 5,000/= hivyo jumla inakuwa tsh elfu ishirini.
Kumbuka mwisho wa kutoa taarifa ya kupewa memory kadi hii ni ijumaa.
Tumia nafasi hii ya kipekee kuboresha maisha yako, kazi zako. biashara zako na hata ufanisi wako. Nafasi hii inakuja mara moja tu, jitahidi sana usiikose.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kuboresha maisha yako.
Kumbuka TUKO PAMOJA.