Mafanikio ni msamiati mpana na una maana tofauti kwa watu tofauti. Pamoja na maana hizi tofauti bado inabaki kwamba mafanikio ni kitu ambacho kila mmoja wetu anakitafuta kwenye maisha. Iwe kufaulu masomo, iwe kupata kazi nzuri, iwe kupanda daraja kazini, iwe kukuza biashara, iwe kulea familia bora na hata iwe kuwa kiongozi bora. Haya yote ni mambo ambayo yanatusukuma kila siku kufanya tunachofanya ili kufikia mafanikio.
Pamoja na kwamba kila mtu anapenda mafanikio, bado ni wachache sana ambao wanafikia mafanikio ya kweli. Wengi wanaishia kuwa kawaida na wakati mwingine kushindwa kabisa.
Nini kinasababisha yote hayo?
Sababu kubwa inayofanya wachache wafanikiwe na wengi washindwe ni kutokujua misingi muhimu ili kufikia mafanikio. Watu wengi hawajui ni vitu gani wanahitaji kuwa navyo au wanahitaji kujua ili kufikia mafanikio.
Kwa kuwa AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA tunataka wewe uweze kufikia mafanikio makubwa sana, tunakuja na siku 30 za mafanikio. Kwa siku 30, kila siku utapata makala moja inayoeleza siri muhimu ya wewe kufikia mafanikio makubwa.
Mafundisho ya siku hizi 30 yanatokana na kitabu, HOW TO ACHIEVE TOTAL SUCCESS IN LIFE ambacho ni kitabu kizuri sana kati ya vingi nilivyosoma mwaka huu. Mafundisho haya yatakuwa kwa lugha rahisi ya kiswahili.
Baada ya siku hizi 30 utakuwa mtu wa tofauti sana na ulivyo sasa. Utaona makosa unayofanya kila siku na yanayokuzuia kufikia mafanikio makubwa na pia utaona fursa nyingi zilizopo mbele yako ambazo hukuwahi kuzijua.
Siku hizi 30 zitabadili kabisa mtazamo wako kuhusu wewe binafsi, maisha na hata mafanikio kwa ujumla. Siku hizi 30 zitaanza tarehe 01 mwezi wa tisa mpaka tarehe 30 mwezi wa tisa, kila siku bila ya kujali mwisho wa wiki au mapumziko. Hizi ni siku 30 za mageuzi katika maisha yako.
Utapata mafundisho haya ya siku 30 kwenye KISIMA CHA MAARIFA na kwa wanachama wa GOLD MEMBER. Kama bado hujawa mwanachama pata UTARATIBU WA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi hayo. Na kama ni mwanachama ila sio wa GOLD jitahidi uweze kuwa GOLD MEMBER.
Kwa yeyote anayetaka kuwa mwanachama ila gharama zinamshinda kulipa kwa pamoja tafadhali tuwasiliane kwa amakirita@gmail.com au 0717396253 na tutaweka utaratibu mzuri wa kuweza kuwa mwanachama. Wengi waliokuwa wameshindwa gharama kwa mara moja tumeshaweka nao utaratibu mzuri na sasa ni wanachama wa GOLD.
Usikose siku hizi 30 za mageuzi kwenye maisha yako, pia mambo mengi mapya yataendelea kukujia kupitia KISIMA CHA MAARIFA.
Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
TUKO PAMOJA NA TUTAKUTANA KILELENI.